
Dar es Salaam. Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya
ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo
atatua nchini.
Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi
katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza
kwamba halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses
Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana
na uzito wa ugeni huo.
Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika
uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa.
“Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za
ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais
huyo,” alisema Malaki.
Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja
sasa na tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa
wakifika kwa nyakati mbalimbali.
“Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa
nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema
Malaki.
Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini
hawakutambua ni mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye
walipelekewa taarifa kuwa ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa
angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.
Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja
itakayombeba, ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi
wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura
ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA).
Malaki alisema maofisa wa Marekani wanaowasili nchini wamekuwa
wakifanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kuwa hali ya usalama
inaimarishwa na kuwaacha wazawa wakifanya shughuli za kawaida.
“Ulinzi ni mkali mno, yapo masharti kadhaa wanayoyataja kuwa yatatumika kwa watu watakaoingia eneo la uwanja au kuisogelea ndege ya Rais Obama. Jamaa wameweka masharti magumu,” alisema.
“Ulinzi ni mkali mno, yapo masharti kadhaa wanayoyataja kuwa yatatumika kwa watu watakaoingia eneo la uwanja au kuisogelea ndege ya Rais Obama. Jamaa wameweka masharti magumu,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema maofisa hao wanakuja kwa makundi na hivi
karibuni lilifika kundi la kusimamia mawasiliano ambayo yatatumiwa
wakati watakapokuwa nchini.
“Pia wamechukua kwa muda karakana ya Shirika la Ndege la Precision
Air iliyoko kwenye eneo la Uwanja wa Ndege. Maofisa wa Usalama wa
Marekani wanataka kufanya shughuli ndani mle,” alisema Malaki.
Pia, ndege mbovu zilizokuwa kwenye maeneo ya uwanja huo zimeondolewa.
Viongozi wa Precision Air hawakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Fadhili
Manongi alisema ni utaratibu wa kawaida kwa karakana kuazimwa wakati
wanapokuja wageni mashuhuri.
“Nafasi ile mara nyingi hutumiwa na maofisa wa usalama pale
wanapokuja wageni mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere,”
alisema.
Alidokeza pia pamoja na ugeni wa Rais Obama, pia kumekuwa kuna presha
ya ugeni wa marais wa nchi mbalimbali duniani wanaokuja kuhudhuria
mkutano wa Smart Partnership unaonza keshokutwa.
Pia wana kazi ya kuwapokea wake za marais wa Afrika watakaokutana na
mke wa Rais Obama, Michelle na mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo,
George Bush, Laura.
Kazi inayofanyika
Ofisa mmoja wa Uwanja Ndege ambaye hakutaka jina lake litajwe,
alisema maofisa hao walifanya ukaguzi wa hali ya juu kwenye sehemu
mbalimbali za uwanja huo wakitumia mitambo maalumu ya kung’amua mabomu.
“Hawa jamaa wako juu sana katika mambo ya usalama maana wana kifaa
cha kuchunguza mabomu hata yaliyo chini ya ardhi,” alisema na kuongeza
kuwa licha ya kukagua uwanja huo, pia walikwenda mbali zaidi na kukagua
maeneo ya jirani.
Mitambo mbalimbali ya shughuli za usalama imefungwa kwenye eneo hilo
la uwanja na maofisa wa Marekani walionekana wakiwa juu ya paa la moja
ya majengo ya uwanja huo wakifunga mitambo katika minara mirefu kwa
ajili ya kuimarisha mawasiliano.
Yavuruga ratiba za ndege
Yavuruga ratiba za ndege
Manongi alisema kampuni za ndege zimeagizwa kufanya mabadiliko ya
ratiba za safari siku atakapowasili Rais Obama ili kutoa nafasi kwa anga
hilo kutumika kwa shughuli za mapokezi yake.
Alisema kampuni zote za ndege zimeshapewa taarifa kuhusu hatua hiyo.
“Kubadilishwa kwa ratiba kunatokea mara kwa mara na huwa tunawapa
taarifa kampuni za ndege mapema ili wajue namna ya kujipanga,” alisema
Manongi.
Kutua Senegal leo
Rais Obama anatarajiwa kuanza ziara yake ya barani Afrika leo na
alitarajiwa kutua Dakar, Senegal saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika
Mashariki.
Akiwa nchini humo, ratiba inaonyesha kuwa atakuwa na mazungumzo na
Rais wa Senegal, Macky Sall kwenye Ikulu ya nchi hiyo. Pia ratiba hiyo
inaonyesha kuwa atakutana na majaji kutoka mikoa yote ya nchi hiyo.
Pia atakwenda katika Kisiwa cha Goree ambacho kiko kwenye Bahari ya
Atlantic na atatembelea Jumba la Makumbusho katika kisiwa hicho ambacho
kilikuwa kituo cha kuhifadhi watumwa waliokuwa wanasafirishwa kutoka
Afrika kwenda Marekani.
“Baada ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria dhifa ya taifa kabla
ya kupumzika kwa muda mfupi na kuanza safari ya kwenda Afrika Kusini,”
ilisema taarifa hiyo ya Ikulu ya Marekani.
Source:Mwananchi
Source:Mwananchi
No comments:
Post a Comment