Sunday, 9 June 2013

Jo achukua pahala pa Damiao kikosi cha Brazil



Brazil imeongeza mshambuliaji Jo katika kikosi chake cha Kombe la Confederations kuchukua pahala pa Leandro Damiao, ambaye ana jeraha la paja la kulia, Shirikisho la Soka la Brazil lilisema mnamo Ijumaa.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 26 anatarajiwa mara moja kwenda Porto Alegre ambapo Brazil itakabiliana na Ufaransa Jumamosi katika mechi yao ya mwisho ya kirafiki kabla ya kuanza kwa Kombe la Confederations Juni 15 dhidi ya Japan.
Straika huyo wa Atletico Mineiro amekuwa katika hali nzuri zaidi tangu arejee Brazil na ameunda ushirikiano muhimu na Ronaldinho na Diego Tardelli.
Kwa sasa, ni mmoja wa wachezaji wawili waliofunga mabao mengi katika Kombe la Libertadores mwaka huu na ana matumaini ya kuongeza mara tatu ambayo amechezea timu ya taifa.
Jeraha hilo la paja ni pigo kubwa kwa Damiao, ambaye alikuwa ametarajiwa kukabili Ufaransa na alitumaini kuwa angetumia Kombe la Confederations kujitangaza akilenga kueleke

No comments:

Post a Comment