Timu ya Taifa ya Morocco jana ilifanikiwa kuifunga timu ya
Taifa ya Gambia kwa magoli 2-0 na kuipiku Tanzania katika msimamo wa
Kundi C.
Mpambano ulikuwa mkali na Morocco walifanikiwa kupata goli la kwanza
katika dakika ya 3 kupitia kwa Barrada na kipindi cha pili Belhanda
akaipatia goli la pili ikiwa ni dakika ya 51 ya mchezo,na kuiacha kabisa
Gambia kuendelea kushika mkia kwa kuwa na pointi moja.
Kwa matokeo hayo Morocco sasa wanapanda hadi nafasi ya pili wakiwa na
pointi 8 wakiachwa kwa pointi mbili na vinara wa kundi hilo Ivory Coast
wenye pointi 10 ambao leo watakuwa wageni wa Timu ya Taifa ya Tanzania
watakapopambana pale Jijini Dar es Salaam.
Pia matokeo hayo yanaifanya timu ya Taifa ya Tanzania maarufu kwa
Taifa Stars kurudi hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 6 ivo itahitaji
kucheza kwa kujituma zaidi ili washinde katika mchezo wa leo na kujiweka
katika nafasi nzuri yakuwania kufuzu kwa kombe la Dunia mwakani 2014
litakalofanyika nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment