Kwa ufupi
Akizungumza jana wakati wa kusaini makubaliano
ya msaada huo ambao umetolewa kupitia Shirika la Misaada la Ujerumani
(GIZ), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick
Utouh, alisema msaada huo wa Euro 3.5 milioni utakwenda katika maeneo
mbalimbali ya ukaguzi na kwamba mradi huo utakuwa wa miaka minne.
Dar es Salaam. Serikali ya Ujerumani imetoa msaada wa zaidi ya
Sh7 bilioni kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za ukaguzi
zinazofanywa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT).
Akizungumza jana wakati wa kusaini makubaliano ya
msaada huo ambao umetolewa kupitia Shirika la Misaada la Ujerumani
(GIZ), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick
Utouh, alisema msaada huo wa Euro 3.5 milioni utakwenda katika maeneo
mbalimbali ya ukaguzi na kwamba mradi huo utakuwa wa miaka minne.
Alisema lengo la msaada huo ni kuboresha utendaji
wa ofisi hiyo na kuhakikisha inatimiza wajibu wake kwa ufanisi katika
ngazi ya kitaifa na kimataifa pamoja na kuboresha uhusiano na wadau
wakuu wa nje. Alisema pia fedha hizo zitasaidia kuikagua Serikali na
misaada wanayopewa na wafadhili ikiwamo Ujerumani.
“Msaada huu umekuja wakati muafaka hasa ikizingatiwa kuwa tangu Julai mwaka jana tumeanza shughuli za ukagu
No comments:
Post a Comment