Sunday, 9 June 2013

Nigeria wafanya mabadiliko tisa kwa ajili ya Kombe la Confeds


Nigeria imefanya mabadiliko tisa kwenye kikosi chake kwa ajili ya Kombe la Confederations kutoka kwa kikosi kilichoshinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika Februari huku kocha Stephen Keshi akiendeleza sera yake ya kupatia nafasi wachezaji chipukizi Ijumaa.
Orodha hiyo, iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Nigeria, inajumuisha wachezaji wanne ambao hawajawahi kuchezea timu ya taifa pamoja na watano ambao walicheza mara ya kwanza ngazi ya kimataifa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mexico wiki moja iliyopita.
Keshi anaonekana kuridhika na safu yake ya ulinzi lakini amefanya mabadiliko makubwa katika safu nyingine huku Victor Moses na Emmanuel Emenike, waliochangia sana kutwaa ubingwa wa bara Afrika Kusini, wakiwa hawachezi.
Nahodha Joseph Yobo, aliyeachwa nje ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika, pia ameachwa nje na uchezaji wake ngazi ya kimataifa unaonekana kufikia ukingoni, huku Peter Odemwingie na Obafemi Martins wakiachwa nje tena.
Keshi alikuwa amekosolewa sana na vyombo vya habari vya nyumbani kabla ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa kuchagua wachezaji wasio na uzoefu, wanaocheza ligi za nyumbani lakini tangu kutwaa ubingwa amenyamazisha wakosoaji.
Nigeria wako katika Kundi B pamoja na Tahiti, Uruguay na Uhispania katika Kombe la Confederations, ambalo linachezwa kuanzia Juni 15 hadi 30.
Kabla ya kuelekea Brazil, watasafiri Namibia kwa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mjini Windhoek mnamo Jumatano.
Kikosi:
Walinda lango: 23-Chigozie Agbim (Enugu Rangers), 16-Austin Ejide (Hapoel Beer Sheva), 1-Vincent Enyeama (Maccabi Tel Aviv)
Walinzi: 5-Efe Ambrose (Celtic), 21-Francis Benjamin (Heartland FC), 3-Elderson Echiejile (Sporting Braga), 6-Azubuike Egwuekwe (Warri Wolves), 12-Solomon Kwambe, 2-Godfrey Oboabona (both Sunshine Stars), 22-Kenneth Omeruo (ADO Den Haag)
Viungo wa kati: 18-Emeka Eze (Enugu Rangers), 10-John Obi Mikel (Chelsea), 13-Fegor Ogude (Valerenga), 4-John Ogu (Academica Coimbra), 17-Ogenyi Onazi (Lazio), 19-Sunday Mba (Enugu Rangers)
Washambuliaji: 9-Joseph Akpala (Werder Bremen), 15-Michael Babatunde (FC Kryvbas), 11-Muhammad Gambo (Kano Pillars), 8-Brown Ideye (Dynamo Kiev), 7-Ahmed Musa (CSKA Moscow), 20-Nnamdi Oduamadi (Varese), 14-Anthony Ujah (

No comments:

Post a Comment