Sunday, 9 June 2013

Oliech anyang'anywa unahodha

mabadiliko katika kikosi chake huku mshambulizi anayecheza Ufaransa, Dennis Oliech akipoteza unahodha.
Amrouche alikuwa amedokezea SuperSport.com Jumanne kwamba alikuwa anatafakari kumteuwa nyota wa Celtic FC alikuwa kinara wa muda kama kiongozi wa kudumu wa kikosi chake mahala pake mchezaji huyo wa Ajaccio.
“Wakati umewadia wa kufanya mabadiliko katika timu hii na ninakuhakikishia ya kwamba Wanyama atabaki kama nahodha wa Harambee Stars hada baada ya kumalizika kwa adhabu ya Dennis Oliech,” kocha huyo alitibua.
Amrouche alikerwa na kufika kwake Oliech kambini akiwa amechelwa pamoja na utovu wa nidhamu nje ya uwanja akiongeza mchezaji huyo wa kutegemewa hakuonyesha kielelezo chema kwa wachezaji wenzake.
Oliech aliteuliwa na mwalimu wa zamani, Jacob ‘Ghost’ Mulee na amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Stars tangu mwaka wa 2002 pale alipojiunga na timu hiyo mara ya kwanza huku akiandikisha rekodi ya mabao mengi zaidi.

No comments:

Post a Comment