Friday, 19 July 2013

PAUL MFEDE 'BOLINGO' - SIMBA ASIYESHINDIKA ALIYESHINDWA NA KIFO - SHUJAA WA CAMEROON MWAKA 1990 KWENYE KOMBE LA DUNIA ALIYEPOTEZA MAISHA BAADA YA KUSHINDWA KULIPIA MATIBABU



Louis Paul Mfede alikuwa gwiji wa soka nchini Cameroon , alikuwa shujaa ndani ya uwanja na balozi mzuri nje ya uwanja .

Fefe aka Bolingo alikuwa sehemu muhimu ya kikosi kilichoipeleka Cameroon kwenye robo fainali ya kombe la dunia mwaka 1990 na kuweka historia ambayo haijafikiwa mpaka hii leo .

Lakini tarehe 10 mwezi uliopita alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 52 kutokana na maradhi ya mapafu kwenye hospitali moja huko Yaounde na sababu za kifo chake zaidi ya maradhi ilikuwa ukweli kuwa alishindwa kugharamikia dawa na matibabu ya maradhi yake . 


Jeneza la Mfede wakati akienda kuzikwa

Ulikuwa ni mwisho wa kuhuzunisha kwa maisha ya mtu ambaye aliifanyia Cameroon makubwa sambamba na watu kama Roger Milla , Thomas Nkono, Libih Thomas, Maboang Kessack na wengineo hasa miaka 23 iliyopita nchini Italia kwenye kombe la dunia.

Mafanikio ya Mfede na wenzie yaliwafanya Wacameroon wote kujawa na matumaini na kumbukumbu ya wengi waliomshuhudia akiwapiga chenga wachezaji watatu pamoja na tabia yake ya kuwafanya wenzie wajiamini hadi kuwafunga Argentina 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa kombe la dunia mwaka 90 haitafutika vichwani mwa watu wa Cameroon.

Pamoja na yote haya, viongozi wa chama cha soka cha Cameroon na wizara ya michezo waliotaarifiwa na mkewe Paul juu ya hali ya mumewe hawakufanya chochote .

Mtoto wa Mfede anayeitwa Frederick alifichua kuwa msaada pekee ulitoka kwa Roger Milla ambaye alisaidia kulipa gharama za hospitali wakati familia yake ikiwa imekosa msaada. Siku ya mazishi yake, waziri wa michezo Adam Garoua alimtunuku Mfede medali ya heshima kwa mchango wake kwa taifa la Cameroon huku akiweka shada la maua kwenye kaburi lake kwenye kijiji cha Nkol-kosse huko Lekie kwenye jimbo la kati la Cameroon lakini watu wamehoji kwanini Mfede hakupewa huduma wakati akiwa mgonjwa huduma ambayo ni muhimu kuliko hata nishani isiyo na maana wakati huu akiwa amekufa.


Kikosi cha Cameroon kilichofanya maajabu 1990 - Mfede aliyechuchuma wa kwanza mkono wa kulia.

Thomas Nkono alilalamika, "Kwanini watu ambao tuliwahi kuitwa mabalozi leo hii maisha yetu yanafifia kwa aibu na shida . Ninapoona watu wachache ambao ni mashabiki halisi wa soka wakiwa wamelizunguka jeneza la Mfede nasikititka huku nikisema kuwa hii ni mbaya kwa shujaa wa taifa . Inauma kuona akiondoka duniani kama mtu ambaye hakuna anayemfahamu."

Thomas Nkono ambaye anaaminika kuwa kipa bora wa afrika kwa miaka yote aliongeza kuwa, "Watu ambao walijitoa kwa ajili ya soka wanapaswa kutambuliwa na serikali lakini kumuona Mfede anakufa mtaani namna hii inaniuma sana."

Beki wa zamani Benjamin Massing alisema, "Ni huruma sana kumuona mwenzetu amekufa kwa namna kama hii akiwa ametelekezwa na kauchwa mwenyewe."







Mfede akimtuliza Rigobert Song baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye moja ya mchezo wa kombe la dunia 1990

 

Pamoja na kukosekana kwa huduma na mazishi ya kitaifa kwa Mfede au the magic foot yaani guu la kushoto la kichawi kama alivyokuwa akifahamika enzi za miaka ya themanini jina ambalo alipewa na mchezaji bora wa afrika mwaka 1980 Jean Manga Onguene atakumbukwa na wenzie kama mtu mwenye furaha na aliwaunganisha wachezaji wenzie .

"Kesi ya Mfede ni kesi ambayo inawakuta wachezaji wengi wa zamani wa Cameroon hasa wale wa miaka ya tisini .

Sisi wanasoka hakuna anayetujali
," anasema mchezaji wa zamani Libih , anaongeza, "Mbaya zaidi hakuna umoja miongoni mwetu kwa kuwa sio serikali pekee ambayo itafanya kila kitu . Ni kweli kuwa tunajitolea maisha yetu kupigania bendera ya taifa letu lakini baadaye tunakuwa watu wa kawaida lazima tukutane na maisha ya baada ya soka. 

Inatia huruma kuwa wachezaji wakubwa hawaweki misingi yoyote ya kulinda maslahi yetu . Tunakimbilia maisha mabaya ambayo hayafahamiki na ndio maana tunapambana kwenye televisheni kwa kuwa tunataka kurudi mahala fulani, inatia huruma na maisha ni magumu, tunapigana sisi kwa sisi badala ya kujenga."

Mchezaji mwingine Youmbi Ayakan ambaye alicheza kwenye miaka ya tisini aliungana na Libih ambapo alisema kuwa kuna haja ya wachezaji kujipanga na kuweka hali zao za baadaye kuwa nzuri zaidi. "Ni muhimu kwa wale wanaocheza sasa na hata wale waliostaafu, wachezaji wengi wa sasa hata hawafahamu kaka zao waliocheza kabla yao, sisi ndio tuliwafanya waote kufikia mahali hapa walipo leo hii lakini hakuna anayefanya kitu kwa ajili yetu."

Suluhisho la tatizo hili kwa mujibu wa Libih ni kwa wachezaji waliostaafu kutumia uwezo wao kuwasaidia wachezaji wachanga ama kuwa viongozi wa chama cha soka na tawala nyingine za michezo na hata kuingia kwenye ukocha

"Kuna haja ya chama cha soka kulinda maslahi ya wachezaji kwa kuwa sisi wote tumefanya makubwa kwa niaba ya taifa na kuna haja ya wanamichezo wote kwa pamoja kulindwa."

SAKATA LA USAJILI WA ROONEY : FAMILIA YAANZA KUATHIRIKA - MKEWE HATAKI WAHAMIE NJE YA NCHI

Sakata la usajili la mshambuliaji WAYNE Rooney jana usiku lilitishia kuivunja familia yake — kwa sababu mkewe wake Coleen hataki kuhamia nje ya nchi hiyo.

Man United jana ilikataa ofa inayotajwa kuwa £20million kutoka Chelsea, mahala ambapo mshambuliaji huyo inasemekana yupo radhi kwenda kwa kuwa Coleen, 27, ataendelea kuwa karibu na wazazi wanaoishi huko Liverpool.
Coleen Rooney with eldest son Kai
Lakini United wanaonekana hawapo tayari kuwauzia silaha wapinzani wao wa moja kwa moja ndani ya ligi kuu ya England - hivyo kufanya kuwepo na uwezekano mkubwa wa uhamisho wa kwenda Paris Saint-Germain kufanikiwa kama Moyes akiamua kumuuza Rooney.
Wayne Rooney at training ground 
Chanzo kimoja cha habari kilisema: “Suala hili la uhamisho wa Rooney linasababisha hali tete baina ya Wayne na Coleen. Hawataki kuhamia nje ya nchi. Lakini ikiwa hatashindwa kuhamia Chelsea basi mambo yatazidi kuwa magumu kwao. 
“Chaguo la kwanza la Wayne ni Chelsea kwa sababu wakihamia kusini mwa nchi bado wataendelea kuwa karibu na Liverpool wakiendesha masaa kadhaa kwenda mahala wazazi wao wanapoishi.
“Lakini United wamesema kwamba, ikiwa watamuuza - itakuwa ni kwa klabu ya nje tu, hivyo PSG wanaweza wakarudi na ofa nzuri. 
"Coleen hataki kabisa kwenda Ufaransa kwa sababu anadhani ni mbali sana na ilipo familia yake, ambao wanamsaidia sana katika kulea wanae Kai na Klay.
"Hivyo ikiwa atauzwa, Wayne itabidi atumie ndege binafsi kutoka Paris-Liverpool, au aende kuishi mwenyewe hotelini.”

Mchana wa jana mke wa Rooney, Coleen alijikuta tena kwenye majibizano makali na baadhi ya mashabiki kwenye mtandao wa Twitter ambao walikuwa wakimtumia meseji ampelekee Rooney kuhusu suala la uhamisho wake - hali ambayo inazidi kuleta hali tete.

WAKATI KOCHA WAO AKIUGULIWA NA MAMA YAKE - MAN CITY WAZIDI KUIMARISHA TIMU YAO - NEGREDO NA JOVETIC WASAJILIWA


MANUEL PELLEGRINI amesafiri kwenda kwao Chile jana usiku wakati Manchester City ikikamilisha usajili wa £39million wa washambuliaji wa wawili.

Kocha huyo aliiacha klabu yake ikiwa kwenye kambi ya mazoezi nchini South Africa kwa sababu anauguliwa na mama yake mazazi.

City wana matumaini Pellegrini, 59, ataungana na kikosi chake tena huko Hong Kong jumanne ijayo — akiungana na washambuliaji wapya wa timu hiyo Alvaro Negredo na Stevan Jovetic.
Negredo akienda kufanyiwa vipimo vya afya
Bosi msaidizi wa klabu hiyo Brian Kidd alisema: “Manuel imembidi arudi nyumbani kwao Chile. Tuna matumaini ataungana nasi tukiwa Hong Kong jumanne lakini hatuna uhakika." 

Mshambuliaji wa kihispaniola Negredo, 27, jana mchana alikuwa jijini Manchester kwenye hosptiali ya Bridgewater akifanyiwa vipimo kukamilisha uhamisho wake wa kutoka Seville kwa ada ya uhamisho ya kuanzia ya £16.4m — huku £4.2m zitalipwa kutokana na kiwango cha mchezaji.
City pia tayari wameshakubalina ada ya usajili ya £22.4 kwa ajili ya mshambuliaji wa Fiorentina Stevan Jovetic.
Mshambuliaji huyo wa Montenegro, 23, atawasili jijini Manchester leo kukamilisha dili hilo la usajili. 
Jovetic alisema: “Mimi bado kijana na nataka kubadilisha maisha yangu ya kisoka.
“City ni timu kubwa na muhimu ndani ya Premier League.
“Nataka kushinda makombe na pia nitakuwa na rafiki yangu mkubwa Matija Nastasic.”

L.A LAKERS YATAKA KUMUUNGANISHA KOBE NA AIDHA LeBRON JAMES AU CARMELO ANTHONY


Timu ya mpira wa kikapu Los Angeles Lakers wanajiandaa kuimarisha timu yao kwa kutaka kumsajili LeBron James au Carmelo Anthony baada ya msimu ufuatao wa ligi, ESPN inaripoti. 
Mastaa wote wawili LeBron na Anthony watakuwa huru msimu ujao ikiwa wataamua kutoongeza mikataba yao ya sasa na vilabu vyao. Kunfi la wachezaji wengine wa kikapu, akiwemo Dwyane Wade, Amar’e Stoudemire na Chris Bosh wana kipengele cha uhuru wa kukatisha mikataba yao, katika mikataba ya miaka mitano waliyosaini mwaka  mapema 2010.
Luol Deng, Danny Granger, Andrew Bogut na Dirk Nowitzki watakuwa huru mwishoni mwa msimu ujao wa ligi ya NBA. Pia L.A Lakers itabidi kufanya uamuzi kuhusu hatma ya Kobe Bryant, ambaye yupo atakuwa anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake msimu huu unaokuja.

LeBron James, ambaye ni mshindi wa tuzo ya NBA Finals MVP, alisema hivi karibuni kwamba hafikirii kabisa kuhusu mkataba wake utakapoisha mnamo mwaka 2014.
Lakers walimpoteza Dwight Howard wakati alipoamua kusaini mkataba wa na Houston Rockets badala ya kuongeza mkataba wa miaka mitano na timu hiyo ya L.A

TOP 100 YA WAFUNGAJI BORA WA LIGI KUU YA ENGLAND - THIERRY HENRY NA HASSELBAINK NDIO WACHEZAJI WA KIGENI PEKEE WALIO NDANI YA TOP 10 -



Wakati zikiwa zimebaki takribani siku 30 kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England - hii ndio listi ya wafungaji bora wa muda wote wa ligi kuu ya England.
Inayoongozwa na Alan Shearer ambaye amefunga jumla ya mabao 260, akifuatiwa na Andy Cole na mfaransa Thierry Henry akishika nafasi ya 3 - huku yeye na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Jimmy Floyd Hasselbaink wakiwa ndio wachezaji pekee kutoka nje ya United Kingdom kuwemo ndani ya Top 10.


JUAN SEBASTIAN VERON ARUDI DIMBANI - AFUATA NYAYO ZA BECKHAM KWA KUTOA MSHAHARA WAKE WOTE KUCHANGIA KITUO CHA KUFUNDISHIA SOKA

Juan Sebastian Veron alimaliza miaka yake 18 ya kucheza soka akiwa na klabu ya Estudiantes mwaka 2012 — hii klabu ambayo alianzia kucheza soka. Veron aliendelea kuitumikia klabu hiyo akiwa kama mkurugenzi wa michezo, huku akicheza soka la mchangani na timu ya ndogo ya Brandsen. Kwa bahati nzuri akiwa na klabu hiyo ndogo walishinda ubingwa wa ligi ya La Plata na inaonekana ubingwa huo umempa hamasa ya kurudi dimbani kiungo wa zamani wa Man United mwenye miaka 38 ambaye sasa ameamua kuichezea klabu ya Estudiantes.
Kutoka Reuters:
Veron, ambaye ni mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Estudiantes, amesaini mkataba wa kuwa mchezaji wa mwaka mmoja na atacheza msimu wote wa 2013-14 wa ligi kuu ya Argentina.
"Sidhani kama nipo kwenye fomu niliyokuwa nayo mwaka  (2009) wakati tuliposhinda ubingwa wa Libertadores Cup, lakini sasa nimehamasika zaidi kurudi uwanjani kwa sababu napenda kucheza soka," alisema Veron alippongea na Radio Del Plataearlier wiki hii.
Pia labda kwa kufuata mfano wa mchezaji mwenzie wa zamani wa Man United - David Beckham, Veron ameamua kwamba atachangia mshahara wake wote kwenye kituo cha soka ambacho alijifunzia soka miaka 20 iliyopita.

NDOTO ZA KUREJEA UNITED ZAZIDI KUFUTIKA - CRISTIANO RONALDO AIWEKA SOKONI NYUMBA YAKE YA JIJINI MANCHESTER


Matumaini ya mashabiki wa Manchester United kuona kipenzi chao Cristiano Ronaldo akirejea kuitumikia klabu hiyo jana yalizidi kupotea baada ya mchezaji huyo kuiweka sokoni nyumba yake aliyokuwa akiishi wakati yupo nchini England kabla ya kujiunga na Real Madrid.
Ronaldo, 28 — aambaye alijiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa £80million mnamo mwaka 2009 — amekuwa akiuhusishwa sana kurejea Manchester United.

Lakini mreno huyo sasa ameiweka sokoni nyumba yake yenye vyumba vitano iliyopo kwenye eneo la Alderley Edge, Cheshire, kwa bei ya £3.75million.

Chanzo kimoja cha habari kilisema: “Mashabiki wa United  mara zote walikuwa wanajua hatua ya Ronaldo kutokuiuza nyumba yake iliyopo jijini Manchester ilikuwa ni kwa sababu alikuwa na mpango wa kurejea mjini labda kujiunga na United, lakini baada ya mwenyewe jana kuiweka sokoni nyumba hiyo - inayoonyesha matumaini ya Ronaldo kurudi Old Trafford yanazidi kufutika.

SERIKALI YAPIGILIA MSUMARI KUSISITIZA TOZO LA KODI YA SIMU LIPO PALEPALE


Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesisitiza uamuzi wa Serikali kuendelea kutoza Sh 1,000 kwa kila mwezi kwa laini ya simu, licha ya kampuni za simu na wanasiasa kupinga.

Akizungumza na mwandishi juzi, Mgimwa alikumbusha wanaolalamikia kodi hiyo, kwamba suala la ulipaji kodi kwa taasisi au watu binafsi, ni la kisheria kulingana na mapato yao na hali halisi iliyopo.

Pia alieleza kushangazwa na matangazo ya baadhi ya kampuni kuhusu utozwaji kodi wananchi akisema wananchi ndio wanataka barabara, maji na umeme vijijini na kodi hizo zinakwenda kutumika huko. 
Kwa mujibu wa Mgimwa, kodi ya laini za simu na ya intaneti, imetengwa ikatumike kusaidia maji na uwezo wa Serikali kupeleka elimu vijijini jambo ambalo ni la maendeleo.
"Wananchi wenyewe wanalalamikia ukosefu wa huduma na baada ya Serikali kupitia na kufanyia kazi changamoto hizo, imeridhia kodi hizo wanakuja watu wanalalamika,"alisema.
Alisisitiza kuwa ongezeko la kodi kwa huduma za intaneti, ni kwa ajili ya kuboresha mfumo wa elimu ambao unalalamikiwa mara kwa mara.




Mgimwa alisema ulipaji kodi unatokana na aina ya biashara na mapato na kutaka kampuni zinazokatwa kodi, kutojilinganisha na kampuni zingine.

Alishangaa wabunge wanaolalamikia ulipaji Sh 1,000 za simu, kwa maelezo kwamba kodi hiyo haikupendekezwa na Serikali, bali Bunge kupitia Kamati ya Bunge lilitaka wananchi wakatwe Sh 1,450.

Baada ya mapendekezo, Mgimwa alisema Serikali ilifanya  uchambuzi na kuamua kupunguza hadi Sh 1,000.   
  
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, jana alisema msimamo wa Serikali ndio wake pia.
Kauli ya Mgimwa inajibu malalamiko ya baadhi ya kampuni, wabunge na vyama vya siasa, kwamba ongezeko hilo linaongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.

Hivi karibuni kampuni za simu na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), walilalamikia kodi hiyo kwamba inaongeza gharama za maisha kwa wananchi.

Mbali na Mnyika, hata CCM kupitia taarifa ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ilitaka kodi hiyo iondolewe na Serikali itafute vyanzo vingine vya mapato.  


Pia Chama cha Watoa Huduma za Mitandao ya Intaneti Tanzania (TISPA), walilalamikia sheria mpya ya kodi na ushuru wa bidhaa katika intaneti, kwamba itachangia ongezeko la gharama za huduma ya intaneti kwa watumiaji wa kawaida.
 
Na Juma Mtanda

MTWARA WANANCHI WACHARUKA WASHAMBULIA KWA MAWE GARI LILILOKUWA LIMEBEBA MABOMBA YA KUSAFIRISHIA GESI

Habari zilizotufikia kutoka mjini Mtwara Zinasema kuwa Gari lililobeba Shehena ya Mabomba ya Kusafirishia gesi kutoka Mjini Mtwara kuelekea Dar limeshambuliwa na mawe na kupelekea dereva Wa lori hilo Kujeruhiwa Vibaya. Lori hilo lilianza kushambuliwa mara baada ya kuingia katika manispaa ya mikinda Mtwara Mjini Sababu ya kushambulia gari hilo ni katika kile kinacho dhihirisha kua wana Mtwara bado hawajakubaliana na hoja ya Serikali ya kutaka Kusafirisha Gesi hiyo kwaajili ya Manufaa ya Nchi.
Lori hilo kwa sasa lipo kituo kikubwa cha polisi Mtwara, Ikiwani wiki moja tu imepita tokeaa watu kadhaa kukamatwa na jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kile kinachodaiwa kusambaza waraka wa kuhujumu miundombinuu yote ya gesi mara tu serikali itakapo anza utekelezaji wake wa ujenzi wa bomba hilo kupeleka dar

Sunday, 14 July 2013

PICHA ZA NDOA YA KIUNGO MAHIRI WA BARCELONA XAVI HERNANDEZ

PREZZO BADO YUKO NA DIAMOND


Mwanamuziki Jackson Makini “Prezzo” ameendelea kumrushia makombora ya maneno Diamond kila anapopata wasaa hasa kupitia kwenye tweeter. Sakata hili limetokana na majigambo ya Diamond kwenye vyombo vya habari kabla ya Tamasha la Matumaini kufanyika kuhusu kumgalagaza Prezzo kwenye show hiyo. Wakati Diamond alikuwa ananogesha tamasha lakini Prezzo ameonekana kutokupendezwa na kauli ya Diamond.

Prezzo alianza mashambulizi dhidi ya Diamond kwa kuweka picha ya gazeti inayowaonesha akiwa na Diamond kwenye habari iliyohusu tamasha hilo na kuandika ‘Hahahaha DomoSeriouly????. Baadaye kidogo akatuma post nyingine inayosema ““U talkin money or u talkin nonsense au anashindana na ndovu?

binti wa miaka 16 /WondaGurl/alitengeneza beat kwenye albam ya jay z


wondagurl in studio with jay z
Moja ya habari zinazizungumzwa sana kwenye mtandao ni producer wa miaka 16  WondaGurl, ambaye ameshiriki katika kutengeneza beat kwenye albam ya Jay Z Magna Carta… Holy Grail. Ambayo imetangazwa  platinum
Ebony Oshunrinde aka  WondaGurl mcanada mwenye asili ya Nigeria  jina jipya katika production  ya beat za hiphop ametengeneza track ya  “Crown,” kutoka kwenye albam ya jay z WondaGurl alianza kutengeneza beats tangu akiwa na miaka 9 alijifunza kupitia video  clip na ilikuwa inspired za timbaland.akiwa na miaka 14 alishriki mashindano ya kutengeneza beats mjini   Toronto/ Battle of the Beatmakers /lakini akaishia robo fainali lakini alishiriki tena mwaka uliofuatia na akawa mshindi wa kwanza  mafanikio alianza kuyapata baada ya kusign   Black Box.
 

Jinsi alivyo kutana na Jay z
WondaGurl alimtumia track  rapper kutoka  Houston Travi$ Scott ambaye alimjibu alimjibu siku chache baadae kwa  kumwambia  ‘nataka kubadilisha maisha yako “I’m about to change your life.” Scott alimsikiliza track hiyo Jay-Z,kasha akampigia na kumwambia  ‘upo kwenye albam ya jay z ,hongera “You are on Jay Z’s album, congratulations.”
WondaGurl  ambaye mama yake ni mnaigiria Jozie Oshunrinde  akizungumzia mafanikio yake amema mama yake alikuwa anasisitizia aendelee kusoma ata baada ya kusinda mashindano ya kutengeneza beats /Battle of the Beatmakers / ‘niliakikisha napewa credits  kwenye kazi zangu coz pila kufanya hivyo kulikuwa na uwezekano mama yangu kutupa vifaa vyangu wa muziki..
Ili kufahamu zaidi unaweza kum follow kupitia @WondaGurlBeats.

Wednesday, 26 June 2013

MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA: CHAMA CHA CHADEMA KUFUTWA KATIKA RAMANI YA SIASA.....!!


JOHN TENDWA




Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Mh. 'John Tendwa' ametaja kukifuta chama cha siasa cha CHADEMA endapo kitabainika kuwa ndio waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013 huko jijini Arusha na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa. Tendwa  ameyasema   hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix cha EATV akijibu swali la mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp  kuhusu  hatua  zitakazochukuliwa baada ya kutokea kwa tukio hilo jijini humo.





Alipoulizwa kama itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo amedai kuwa hawezi kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kufanya mapinduzi ya kalamu. Baada ya kauli hii ya Mh. 'Tendwa' mijadala kadhaa iliibuka kwenye mitandao hususani kwenye mtandao wa jamiiforum wakikosoa kauli hiyo.

ZINEDINE ZIDANE ATEULIWA KOCHA MSAIDIZI WA REAL MADRID - ATAMBULISHWA PAMOJA NA CARLO ANCELOTTI


Real Madrid wamemtambulisha rasmi kocha wao mpya Carlo Ancelotti na pia wametangaza kwamba Zinedine Zidane na Paul Clement watakuwa ndio makocha wasaidizi.

Ancelotti alitambulishwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu na raisi wa klabu hiyo Florentino Perez mapema leo mchana.
 
Ancelotti atasaini rasmi mkataba wa miaka mitatu na Madrid July 3 akitokea Paris St Germain.



AFANDE SELE NAE AFUNGUKA KUHUSU SAKATA LA OMMY DIMPOZ KUMTUKANA ALBERT MANGWAIR


MSANII wa muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi 'Afande Sele' amuombea msamaha msanii wa muziki Omary Faraja 'Ommy Dimpozi' kutokana na kauli yake aliyeitoa inayodaiwa kumkashifu marehemu Alberty Mangwea 'Ngwair'.

Msamaha huo umetokana na kauli aliyeitoa msanii Ommy Dimpozi kudai kuwa hawezi kufa maskini kama msanii Ngwair.

Afande Sele alidai kuwa kauli hiyo haikuwa mbaya ingawa watanzania hawakuilewa hivyo Ommy ametereza ulimi na anapaswa kusamehewa kama binadamu anapokosea.

Alisema kauli yake ilikuwa inamaanisha wasanii wanatakiwa wapate haki za msingi na siyo kutumiwa huku wengine wakiendelea kunufaika na wao kudidimia na hali ngumu ya kimaisha.

"Hatuwezi kuendelea kufanya hivyo mimi namuombea msamaha kwa watanzania kauli yake ilikuwa na lengo zuri ila ameshindwa kuifikisha vyema hivyo ameteleza inabidi tumsamehe ili mambo mengine yaendele" alisema Sele.

Wakati huo huo bado ile  kauli anayodaiwa kuitoa msanii huyo Ommy Dimpozi' inaendelea kumtesa na kusababisha kushindwa kuwapa burudani mashabiki zake.

Ommy  Dimpozi alipata wakati mgumu baada ya kufanyiwa fujo na mashabiki alipokuwa akifanya shoo pamoja na wasanii wenzake walioshiriki katika Tuzo za Kilimanjaro mwaka huu wakiwa mjini Dodoma.

Msanii huyo anadaiwa kutoa kauli hiyo hivi karibuni ambapo alisema hataki kufa masikini kama ilivyokuwa kwa msanii wa Hip hop Albert Magwear.

Kauli hiyo iliwachukiza baadhi ya mashabiki wa muziki waishio mjini Dodoma ambapo msanii Magwear alisoma na kukulia katika mji huo.

Msanii huyo atazidi kuwa na wasiwasi kwa baadhi ya mikoa atakayozunguka kufanya shoo zake ikiwemo mkoa wa Morogoro ambapo ndio familia ya msanii huyo inapoishi.

Alipotafuta na mwandishi wa habari hili kuzungumzia ishu hiyo Dimpozi alisema hayuko tayari kusema chochote kinachohusiana na shoo yake ya Dodoma na hataki kumzungumzia Magwear.

ASANTE KWA KUNIPA MCHANGO WAKO WA KUPITIA BLOG HII




MAJAMBAZI WAVAMIA KITUO CHA MAFUTA ORYX MAKAMBAKO WAPORA MAMILIONI YA SHILINGI WAUA WALINZI WAWILI WAJERUHI MENEJA


Focas Malengo Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe
.....................................................................................................................

Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wakiwa na silaha mbali mbali zikiwemo wa moto wamevamia kituo cha Mafuta cha Oreyx kilichopo mjini Mkambako mkoa wa Njombe na kufanya mauwaji ya kinyama kwa walinzi wawili na kujeruhi mmoja kabla ya kupora kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 7

Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana .

Mashuhuda hao walisema kuwa majambazi hao wawili wakiwa na usafiri wa piki piki ambapo walifika katika kituo hicho kwa ajili ya kununua mafuta ya Tsh 5000 na wakati wakiendelea kuhudumiwa ghafla walianza kuwashambulia walinzi kwa risasi na kuwaua walinzi wawili na kumjeruhi meneja wa kituo hicho.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Focas Malenge amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja waliouwawa kuwa ni Jonas Mpogole na Chesco Sanga ambao ni walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Makambako .

Mbali ya kuwaua walinzi hao wawili pia majambazi hayo yalimjeruhi kwa risasi meneja wa kituo hicho Jonas Msenyi na kupora fedha zaidi ya Tsh milioni 7

Alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwasaka majambazi hayo ikiwa ni pamoja na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo la polisi

NIKUMBATIE 'AM READY TO FLY' FEAT. FUNDI SAMWELI IJUMAA HII NDANI YA AMBASSADORS LOUNGE

POLISI JIJINI DAR WAKAMATA WATU WAWILI WAKIWA NA BASTOLA KATIKA PIKIPIKI


Askari kanzu (kulia) akiwa ameshika bastola aliyokutwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usaji T 961 CJW katika mtaa wa Makunganya jirani kabisa na benki ya Posta jijini Dar es Salaam mchana huu. Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ujambazi wa kutumia pikipiki Polisi wameimarisha ulinzi na hasa katika maeneo ya mabenki.
TOA MAONI YAKO HAPA

Ulinzi wa Obama Dar

obama

Dar es Salaam. Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini.
Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.
Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa.
“Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,” alisema Malaki.
Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa nyakati mbalimbali.
“Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.
Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.
Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Malaki alisema maofisa wa Marekani wanaowasili nchini wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kuwa hali ya usalama inaimarishwa na kuwaacha wazawa wakifanya shughuli za kawaida.
“Ulinzi ni mkali mno, yapo masharti kadhaa wanayoyataja kuwa yatatumika kwa watu watakaoingia eneo la uwanja au kuisogelea ndege ya Rais Obama. Jamaa wameweka masharti magumu,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema maofisa hao wanakuja kwa makundi na hivi karibuni lilifika kundi la kusimamia mawasiliano ambayo yatatumiwa wakati watakapokuwa nchini.
“Pia wamechukua kwa muda karakana ya Shirika la Ndege la Precision Air iliyoko kwenye eneo la Uwanja wa Ndege. Maofisa wa Usalama wa Marekani wanataka kufanya shughuli ndani mle,” alisema Malaki.
Pia, ndege mbovu zilizokuwa kwenye maeneo ya uwanja huo zimeondolewa. Viongozi wa Precision Air hawakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Fadhili Manongi alisema ni utaratibu wa kawaida kwa karakana kuazimwa wakati wanapokuja wageni mashuhuri.
“Nafasi ile mara nyingi hutumiwa na maofisa wa usalama pale wanapokuja wageni mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere,” alisema.
Alidokeza pia pamoja na ugeni wa Rais Obama, pia kumekuwa kuna presha ya ugeni wa marais wa nchi mbalimbali duniani wanaokuja kuhudhuria mkutano wa Smart Partnership unaonza keshokutwa.
Pia wana kazi ya kuwapokea wake za marais wa Afrika watakaokutana na mke wa Rais Obama, Michelle na mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, George Bush, Laura.
Kazi inayofanyika
Ofisa mmoja wa Uwanja Ndege ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema maofisa hao walifanya ukaguzi wa hali ya juu kwenye sehemu mbalimbali za uwanja huo wakitumia mitambo maalumu ya kung’amua mabomu.
“Hawa jamaa wako juu sana katika mambo ya usalama maana wana kifaa cha kuchunguza mabomu hata yaliyo chini ya ardhi,” alisema na kuongeza kuwa licha ya kukagua uwanja huo, pia walikwenda mbali zaidi na kukagua maeneo ya jirani.
Mitambo mbalimbali ya shughuli za usalama imefungwa kwenye eneo hilo la uwanja na maofisa wa Marekani walionekana wakiwa juu ya paa la moja ya majengo ya uwanja huo wakifunga mitambo katika minara mirefu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano.
Yavuruga ratiba za ndege
Manongi alisema kampuni za ndege zimeagizwa kufanya mabadiliko ya ratiba za safari siku atakapowasili Rais Obama ili kutoa nafasi kwa anga hilo kutumika kwa shughuli za mapokezi yake.
Alisema kampuni zote za ndege zimeshapewa taarifa kuhusu hatua hiyo.
“Kubadilishwa kwa ratiba kunatokea mara kwa mara na huwa tunawapa taarifa kampuni za ndege mapema ili wajue namna ya kujipanga,” alisema Manongi.
Kutua Senegal leo
Rais Obama anatarajiwa kuanza ziara yake ya barani Afrika leo na alitarajiwa kutua Dakar, Senegal saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.
Akiwa nchini humo, ratiba inaonyesha kuwa atakuwa na mazungumzo na Rais wa Senegal, Macky Sall kwenye Ikulu ya nchi hiyo. Pia ratiba hiyo inaonyesha kuwa atakutana na majaji kutoka mikoa yote ya nchi hiyo.
Pia atakwenda katika Kisiwa cha Goree ambacho kiko kwenye Bahari ya Atlantic na atatembelea Jumba la Makumbusho katika kisiwa hicho ambacho kilikuwa kituo cha kuhifadhi watumwa waliokuwa wanasafirishwa kutoka Afrika kwenda Marekani.
“Baada ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria dhifa ya taifa kabla ya kupumzika kwa muda mfupi na kuanza safari ya kwenda Afrika Kusini,” ilisema taarifa hiyo ya Ikulu ya Marekani.
Source:Mwananchi

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU...YADAI POLISI WANARUHUSIWA KUPIGA NA KUUA KISHERIA



Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.


Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.

“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.


Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.


Aliyataja mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia madhara makubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia mtu anayetenda tendo ovu la kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume na maumbile.

Pia kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku au unyang’anyi wa kutumia silaha au kuchoma nyumba moto au kufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai wa mtu au mali.


Alieleza kuwa Kifungu cha 18 na 18(A) cha Sheria ya Adhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.


Kauli hiyo ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi, ilitolewa ikiwa ni ufafanuzi wa jibu la swali la nyongeza lililoulizwa bungeni Mei 28,2013 na Rashir Ally Abdalah (Tumbe-CUF), ambapo Silima alisema mauaji yanayofanywa na askari polisi ni mauaji ya kisheria. 


Kutokana na kauli hiyo, Mbunge wa Wawi, Hamad Rashi Mohammed aliomba mwongozo wa spika kupata ufafanuzi wa kauli hiyo, na jana Silima kutoa kauli ya Serikali kujibu mwongozo huo.

“Ikumbukwe pia kuwa, kifungu cha 29 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi Sura322, pamoja na Kanuni za Kudumu za Utendaji za Jeshi la Polisi Na274, vinampa haki ya kisheria askari polisi kubeba na kutumia silaha za moto ikiwamo bunduki na mabomu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku..,”alisema Silima.


Alifafanua kwamba katika kutafsiri sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ikiwamo alizozitaja, mahakama katika nyakati tofauti imetoa msimamo wa kisheria juu ya suala hilo.


Akitoa mfano alisema: “Mathalan katika kesi ya Seif Mohamed Senzagala dhidi ya Jamhuri ya mwaka 1994 kama ilivyonukuliwa na Tanzania Law Report ukurasa wa 122, ambapo mshitakiwa (mwomba rufaa) alimjeruhi kwa panga mlalamikaji ambaye alimfuata nyumbani kwake na kuanza kumshambulia.”


Alisema katika kesi hiyo,mahakama ya rufaa pamoja na kuridhia uamuzi wa mahakama ya awali wa kumtia hatiani kwa kutumia nguvu kupita kiasi, ilibainisha kuwa mshtakiwa hakustahili adhabu kwani alitenda kosa lile wakati akijihami dhidi ya mashambulizi toka kwa mlalamikaji.

“Kwa msingi huo, tarehe 28 Mei, 2013 wakati nikijibu swali Na 290, nilitumia maneno ‘mauaji yanayofanywa kisheria’ nikimaanisha mauaji yanayotokea katika mazingira niliyoeleza..,”alisema Silima.

Hata hivyo alisema siyo nia ya Serikali kuhalalisha vitendo vya matumizi mabaya ya silaha ambavyo vinaweza kufanywa na askari wasio waadilifu.

Alibainisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kuheshimu haki za raia na kutumia busara kutatua migogoro.

Hata hivyo, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imelaani kauli ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi iliyoitoa jana na kueleza kuwa haikubaliani nayo kwa kuwa inatoa baraka kwa polisi kuendeleza mauaji ya raia.

Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kikao cha bunge kuahirishwa, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani wa kambi hiyo rasmi, Vicent Nyerere alisema kauli hiyo ingekuwa na uthabiti kama askari polisi wangekuwa waadilifu.


“Kauli ingekuwa thabiti kama polisi wangekuwa waadilifu. kabla ya kutoa kauli hiyo, Serikali ilitakiwa kuchuja miongoni mwa askari wa jeshi la polisi, wa ngazi zote na kuwaondoa wasio waaadilifu ndipo wakatoa kauli hiyo wananchi wataielewa Serikali,”alisema Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini(Chadema).


Kwa upande wake, Mbunge wa Ole, (CUF) Rajab Mbarouk Mohammed akizungumzia kauli hiyo ya Serikali alisema kuwa majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima ni ya kisiasa.


Alisema kwamba kauli hiyo ni mwendelezo wa kauli iliyotolewa Alhamisi iliyopita na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwataka pilisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote watakaokaidi kutii sheria.


“Hakuna mwenye haki ya kuua, kuua ni kuua tu. Mahakama pekee ndiyo ina haki ya kuhukumu kifo baada ya kumtia hatiani mshtakiwa husika. Lakini kuwa polisi wanafundishwa utii, siyo kuua,”alisema Rajab.

Alifafanua kuwa kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao na kwamba kuruhusiwa kujihami haimaanishi kuua raia.
Nao Wabunge Aeshi Hilaly na Aly Keissy walisema ni vizuri raia wakatii mamlaka iliyopo na kutekeleza utii wa sheria bila shuruti.

Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu alisema: “Maoni yangu haki za watuhumiwa lazima ziheshimiwe.”

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS), Francis Stola alisema hakuna sheria inayompa mamlaka askari polisi kutumia nguvu za ziada ikiwemo kupiga raia pindi anapotekeleza majukumu yake,isipokuwa tu anaweza kutumia nguvu kiasi iwapo raia anayekabiliana naye anaonyesha vitendo vya kukaidi amri ama kuhatarisha usalama.


Stola ambaye alikuwa akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na kauli bungeni alisema kuwa kwa kufuata sheria polisi haruhusiwi kupiga raia. “ Ukisoma sheria hakuna mahala utakuta kuna neno limeandika piga…. Askari polisi anachoweza kufanya ni arrest(kamata) na siyo vinginevyo, hana mamlaka kabisa ya kupiga raia”

Alisema sheria imetamka wazi kuwa kunapojitokeza hali yoyote inayopaswa kdhibitiwa na vikosi vya ulinzi, nguvu inayopaswa kutumika ni ile ya kawaida na kwamba kitendo cha kutumia risasi za moto ama kupiga raia ni ukiukwaji wa sheria za nchi.

Alisema polisi anapaswa kutoa mwongozo kwa raia kumwelekeza jambo la kufanya iwapo kunajitokeza hali ya sintofahamu,lakini hapaswi kutumia nguvu kupita kiasi ikiwemo kuwapiga raia

“ Sheria inasema wazi kwamba panapojitokeza hali yoyote korofi, polisi wanatakiwa kutumia nguvu ya kawaida tu kukabiliana na hali hiyo na wala siyo kutumia silaha za moto… silaha za moto zinaweza kutumika tu iwapo kunajitokeza tukio ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa maisha ama mali isipotee” alisema

Kuhusu wananchi kufanya maandamano, rais huyo alisema maandamano ni haki ya msingi ya kila raia,lakini yanafanyika katika utaratibu maalumu. “ maandamano ni haki ya kila raia lakini panapaswa kuwa na utaratibu maalumu…. Kama kunajitokeza maandamano ambayo hayana utaratibu polisi wanapaswa kutumia reasonable force (nguvu ya kawaida) kudhibiti maandamano hayo na wala siyo kutumia nguvu za ziada.
 Mwananchi:

Monday, 24 June 2013

CHIGWA COMING SOON..........!!!!!!!!!!!!!!!!1


MwanaFA..AJUTA KUANZISHA BIFU NA JIDE,,APOTEZA MASHABIKI,HANA RAHA AAMUA KUFUNGUKA..SOMA ALICHOKIANDIKA HAPA


Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
 


Mwanamuziki Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, amepata wakati mgumu kwa kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee, baada ya kuliruka jina hilo alipokuwa akiimba wimbo wa Mabinti ambao ndani yake
kuna jina la Jay Dee.

Tofauti na ilivyozooeleka katika wimbo wa Mabinti, kwa mara ya kwanza Mwana FA aliruka jina la mwanamuziki Lady Jay Dee ‘Anaconda’, hali iliyowafanya mashabiki wamtake arudie tena na kutenda haki.

Mwana FA alisita kwa muda na baadaye aliamua kurudia wimbo huo na alipofika katika kipengele cha kumtaja Jide aliimba kwa kumtaja, hali iliyoufanya ukumbi huo ulipuke kwa shangwe na mashabiki kumtaka arudie tena na tena.

Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.

Awali shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400 tu. Lakini mpaka inafika saa nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa kwa shoo hiyo watu waliokuwa wamefika walikuwa kama 250 tu.

Thursday, 20 June 2013

KAWA HUJAWAI TAZAMA PICHA ZA UTUPU ZA VIDEO QUEEN WA JAMBO JAMBO YA STEVE R&B



WAKATI mabinti wengi hasa mastaa wa Bongo wakijuta baada ya picha zao za utupu walizopigwa na wapenzi wao kuvuja, kwa msanii mrembo aliyepamba video ya wimbo wa Bongo Fleva uitwao Jambojambo wa msanii Steve R&B, Aisha Firozi ‘Sapna’ ni kawaida kwani hujifotoa mwenyewe.

Chanzo makini cha Risasi kimewasilisha folda lenye picha za kutosha za mrembo huyo akiwa mtupu huku kikieleza kwamba ni mchezo wake kujipiga mwenyewe picha hizo.


Kwa sharti la kutochorwa jina lake , chanzo hicho ambacho kipo aribu na Sapna kilisema: “Yule ni mtu wangu wa karibu sana, lakini tabia yake kwa kweli huwa siipendi kabisa. Anajipiga picha chafu mwenyewe, kwake ni starehe kubwa, huwezi kuamini.”

Kikiendelea ufunguka zaidi, chanzo hicho kilipasha kuwa, picha hizo amejipiga hivi karibuni nyumbani kwa rafiki yake aitwaye Doreen, Tabata - Magengeni jijini Dar es Salaam, ambapo alikuwa akiishi naye.

KAULI YA SAPNA.....
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni; Sapna alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu kunaswa kwa picha hizo, kwanza alishangaa lakini akakiri kuzitambua.

“Hizo kweli ni picha zangu na nilijipiga mwenyewe sasa sijui wewe umezipataje na zimefi kaje huko kwenu? Mimi nilipiga kwa masilahi yangu mwenyewe, huwa natamani sana kujiangalia jinsi umbo langu lilivyo, ndiyo maana niliamua kujipiga na si vinginevyo.


“Kila mtu na maisha yake na mimi sikuwa na dhamira mbaya kujipiga picha hizo zaidi ya kujiangalia tu nilivyo,” alisema Sapna.

Sunday, 16 June 2013

Shilole aalikwa kwenda kupiga shoo marekani. Kuondoka hivi karibuni

Shilole aalikwa kwenda kupiga shoo marekani. Kuondoka hivi karibuni
Mwigizaji na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Zena Mohamedi ama Shilole amepata mwaliko wa kwenda nchini Marekani kufanya shoo za mziki hivi karibuni.
Akizungumza na mwandishi wetu tokea ukumbi wa blue pearl wakati wa tuzo za filamu nchini Shilole amesema kuwa yupo kwenye maandalizi ya mwisho kwa ajili ya shoo hiyo ambayo anatarajiwa kuifanya kwenye miji miwili nchini humo.

WANAKILINGE SASA MBEYA WAKAZI WA MBEYA KAZI KWENU KUSIKIA MITAMBAO YA WANAHARAKATI HAO

Mbeya The Green City tarehe 21st June 2013 Nikki Mbishi,One the incredible na Songa watakuwa Club The Vibe,tukutane pale!!!

MLIPUKO WAMKATA VIGANJA MWENDESHA PIKIPIKI DAR...


Mkazi wa Mbagala Chemichem, Abdul Said ambaye ni mwendesha pikipiki amekatika viganja vya mikono miwili baada ya kulipukiw a na kitu alichopewa kushika.
Hata hivyo Said anashikiliwa na polisi na mwenzake mwingine ambaye hakutajwa jina baada ya kukamatwa katika maeneo ya Mbagala jana saa 6:00 usiku.
Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova, alisema watu hao wawili walikamatwa katika maeneo hayo huku wenzao wawili wakipata upenyo na kukimbia.
Alisema dereva huyo wa pikipiki ambaye alikabidhiwa kitu mkononi ambacho ghafla kililipuka na kumkata viganja vya mikono yote miwili.
Alisema jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wengine wawili bado zinaendelea na waliokamatwa wanashikiliwa kwa mahojiano.
Katika hatua nyingine, Kamanda Kova alisema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa makosa mbalimbali ya unyang’anyi kwa kutumia silaha Moshi Omari akiwa na pikipiki aina ya Honda Bajaj yenye namba T607 AQD ambayo ni ya wizi.
“Vilevile katika kuendeleza doria za kuimarisha ulinzi tumewakamata watuhumiwa wawili kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha ambao wameshiriki katika matukio mengi ya uhalifu hapa jijini,” alisema Kamanda Kova.
Aliwataja watu hao kuwa ni Jovin Deofin na Juma Athuman ambao wote ni wakazi wa Kongowe, Wilaya ya Temeke.

Ujerumani yampiga jeki mkaguzi mkuu wa Serikali

Kwa ufupi
Akizungumza jana wakati wa kusaini makubaliano ya msaada huo ambao umetolewa kupitia Shirika la Misaada la Ujerumani (GIZ), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, alisema msaada huo wa Euro 3.5 milioni utakwenda katika maeneo mbalimbali ya ukaguzi na kwamba mradi huo utakuwa wa miaka minne.
Dar es Salaam. Serikali ya Ujerumani imetoa msaada wa zaidi ya Sh7 bilioni kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za ukaguzi zinazofanywa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT).
Akizungumza jana wakati wa kusaini makubaliano ya msaada huo ambao umetolewa kupitia Shirika la Misaada la Ujerumani (GIZ), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, alisema msaada huo wa Euro 3.5 milioni utakwenda katika maeneo mbalimbali ya ukaguzi na kwamba mradi huo utakuwa wa miaka minne.
Alisema lengo la msaada huo ni kuboresha utendaji wa ofisi hiyo na kuhakikisha inatimiza wajibu wake kwa ufanisi katika ngazi ya kitaifa na kimataifa pamoja na kuboresha uhusiano na wadau wakuu wa nje. Alisema pia fedha hizo zitasaidia kuikagua Serikali na misaada wanayopewa na wafadhili ikiwamo Ujerumani.
“Msaada huu umekuja wakati muafaka hasa ikizingatiwa kuwa tangu Julai mwaka jana tumeanza shughuli za ukagu

ASANTE MAMA KWA KUTAMBUA HILO(JOYCE BANDA)


Today we celebrate the life of an African Child. While celebrating the life of an African Child, I believe we have a collective responsibility in eliminating harmful social and cultural practices affecting children in our communities.

I want to ensure everyone that my government will continue to prioritise the welfare of children in this country . We will continue to implement the Safe Motherhood initiatives as their outcomes have proved to be a success in promoting the safety of mothers and children. We will continue to implement the Economic Recovery Plans as the benefits are proving to reduce poverty at household level especially when prices of essential things like fuel have gone down.

I have also felt motivated to accelerate the implementation of the Mudzi Transformation Trust Initiative which is meant to bring the social and economic benefits per family because this is another way of combating poverty.

Let me also assure everyone that our government will continue to implement projects that will address issues of hunger and malnutrition and policies that will promote access to education for our children. We have a zero tolerance stance with regards to harmful practices on children ie child labour, child abuse and neglect because the welfare of children in this country is our number one priority.

As a matter of priority, we will listen to everyone on how best we can work together to make the lives of children better in this country because we are a listening government and because we are very passionate about children.

I take this opportunity to profoundly thank everyone committed to uplift the lives of children in this country. Your contribution is what brings joy to children, please continue with this selfless spirit of doing the best for children.

In my view, a child is like a garden, when one takes care of the garden it becomes glorified with beautiful flowers and landscapes making the entire community proud. Therefore I urge all of us to do our best, children are the future of this nation.

Have a blessed Sunday everyone .

And may God bless your children!

Dr Joyce Banda
President
Republic of Malawi