Timu ya mpira wa kikapu Los Angeles Lakers wanajiandaa
kuimarisha timu yao kwa kutaka kumsajili LeBron James au Carmelo
Anthony baada ya msimu ufuatao wa ligi, ESPN inaripoti.
Mastaa
wote wawili LeBron na Anthony watakuwa huru msimu ujao ikiwa wataamua
kutoongeza mikataba yao ya sasa na vilabu vyao. Kunfi la wachezaji
wengine wa kikapu, akiwemo Dwyane Wade, Amar’e Stoudemire na Chris Bosh
wana kipengele cha uhuru wa kukatisha mikataba yao, katika mikataba ya
miaka mitano waliyosaini mwaka mapema 2010.
Luol
Deng, Danny
Granger, Andrew Bogut na Dirk Nowitzki watakuwa huru mwishoni mwa msimu
ujao wa ligi ya NBA. Pia L.A Lakers itabidi kufanya uamuzi kuhusu hatma
ya Kobe Bryant, ambaye yupo atakuwa anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa
mkataba wake msimu huu unaokuja.
LeBron
James, ambaye ni mshindi wa tuzo ya NBA Finals MVP, alisema hivi
karibuni kwamba hafikirii kabisa kuhusu mkataba wake utakapoisha mnamo
mwaka 2014.
Lakers walimpoteza Dwight
Howard wakati alipoamua kusaini mkataba wa na Houston Rockets badala ya kuongeza mkataba wa miaka mitano na timu hiyo ya L.A
No comments:
Post a Comment